Je, Siku ya Mazingira Duniani ni nini?

Jukwaa la kuchukua hatua

Siku ya Mazingira Duniani ni siku ya Umoja wa Mataifa ya kuhimiza ufahamu duniani kote na hatua za kulinda mazingira yetu. Tangu ianze mwaka wa 1974, tukio hilo limekua na kuwa jukwaa la kimataifa la kufikia umma ambalo linaadhimishwa sana katika nchi zaidi ya 100.

Siku ya watu

Zaidi ya yote, Siku ya Mazingira Duniani ni "siku ya watu" ya kufanya kitu cha kutunza Ardhi. "Kitu" hicho kinaweza kuwa mtaani, kitaifa au ulimwenguni mwote. Inaweza kuwa hatua ya mtu mmoja au inayohusisha umati. Kila mtu ni huru kuchagua.

Mada

Kila Siku ya Mazingira Duniani imeandaliwa kwa mujibu wa mda ambayo inazingatia tahadhari fulani ya mazingira. Mada ya 2019 ni "Uchafuzi wa hewa".

Mahali pa tamasha

Kila Siku ya Mazingira Duniani ina nchi tofauti zinazosimamia tamasha, ambapo sherehe rasmi hufanyika. Kuzingatia nchi inayosimamia tamasha husaidia kuonyesha changamoto za mazingira ambayo inakabiliwa nayo na huunga mkono jitihada za duniani kote za kukabiliana nazo. Nchi inayoandaa tamasha ya mwaka huu ni Uchina.

Usajili

Katika miaka ya hivi majuzi, mamilioni ya watu wamehusika katika maelfu ya shughuli zilizosajiliwa duniani kote. Tafadhali jisajili hapa ili tuweze kukufahamisha juu ya kile kinachoendelea kutokea.

Coral images courtesy of The Ocean Agency, USFWS, Coral Reef Image Bank, XL Catlin Seaview Survey