Ni nini kinachosababisha uchafuzi wa hewa?

Kiasi cha hewa chafu tunayopumua hutegemea mambo mengi kama vile, uwezo wa kupata nishati safi ya kupikia na kupasha joto wakati wa mchana pamoja na hali ya anga. Nyakati za pilkapilka nyingi bila shaka ni chanzo cha uchafuzi katika eneo, lakini uchafuzi wa hewa unaweza kusafiri umbali mrefu, wakati mwingine kuvuka mabara kwenye mitindo ya hali ya anga ya kimataifa.

Hakuna mtu aliye salama kutokana na aina hii ya uchafuzi, ambayo husababishwa na vyanzo vitano vya wanadamu. Vyanzo hivi hutoa aina mbalimbali ya vitu ikiwa ni pamoja na kaboni monoksidi, kaboni dioksidi, naitrojeni dioksidi, naitrojeni oksidi, gesi ya ozoni ya safu ya chini kwenye ardhi, chembechembe ndogo, salfa dioksidi, haidrokaboni, na risasi–ambazo zote zinadhuru afya ya binadamu.

Nyumbani

Chanzo kikuu cha uchafuzi wa hewa nyumbani ni kuchoma visukuku ndani ya nyumba, mbao na visukuku vingine vinavyoweza kutumiwa tena ili kupika, kupasha joto na kuandaa mwangaza. Kila mwaka, vifo vya mapema milioni 3.8 hivi,husababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa, idadi kubwa ya vifo hivyo hutokea katika nchi zinazoendelea.

Nchi 97 kati ya 193 zimeongeza asilimia ya nyumba zinazoweza kupata visukuku safi  vya kuchoma kwa zaidi ya asilimia 85. Hata hivyo, watu bilioni 3 huendelea kutumia visukuku vilivyoganda na mioto iliyo wazi kwa ajili ya kupika, kupasha joto, na kuandaa mwangaza. Kutumia jiko na visukuku visafi vya kisasa, kunaweza kupunguza hatari ya magonjwa na kuokoa maisha.

Kiwanda

Katika nchi nyingi, uzalishaji wa nishati ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa hewa. Viwanda vya kuchoma makaa ya mawe huchangia pakubwa, ilhali jenereta zinazotumia dizeli ni hangaiko linalozidi kuongezeka katika maeneo ambayo hayajaunganishwa na umeme. Shughuli za viwanda na matumizi ya umajimaji katika viwanda vya kemikali na vya kuchimba madini, pia huchafua hewa.

Sera na programu zilizonuiwa kuongeza matumizi mazuri ya nishati na uzalishaji wa vyanzo vinavyoweza kutumiwa kiuendelevu, huchangia moja kwa moja ubora wa hewa ya nchi. Kufikia sasa nchi 82 kati ya 193 zina mambo yanayochochea uwekezaji katika uzalishaji wa nishati inayotumiwa kiuendelevu, uzalishaji safi, matumizi mazuri ya nishati na udhibiti wa uchafuzi.

Uchukuzi

Sekta ya uchukuzi ulimwenguni pote huchangia karibia robo ya hewa yenye kaboni dioksidi inayohusiana na nishati na kiwango hiki kinazidi kuongezeka. Gesi taka zinazotoka kwa usafiri wa uchukuzi zimehusishwa na vifo vya mapema takribani 400,000. Karibu nusu ya vifo vyote vinavyosababishwa na uchafuzi wa hewa kutoka kwa usafiri wa uchukuzi husababishwa na hewa chafu ya dizeli, ilhali wale wanaoishi karibu na barabara kuu zenye msongamano wanaweza kuathirika kwa zaidi ya asilimia 12 na kupatikana na athari za kiakili.

Kupunguza hewa chafu kutoka kwa magari ni njia muhimu ya kuingilia kati ili kuboresha ubora wa hewa, hasa katika maeneo ya mjini. Sera na viwango ambavyo hutaka matumizi ya visukuku safi zaidi na magari yaliyoboreshwa kutoa hewa chafu kulingana na viwango vilivyopo zinaweza kupunguza hewa chafu kutoka kwa magari kwa asilimia 90 au zaidi.

Kilimo

Kuna vyanzo viwili vikuu vya uchafuzi wa hewa vinavyosababishwa na kilimo: mifugo, wanaotoa gesi ya mitheni na amonia, na kuchoma taka ya kilimo. Gesi za mitheni huchangia gesi ya ozoni ya safu ya chini kwenye ardhi, inayosababisha ugonjwa wa pumu na magonjwa mengine ya mfumo wa kupumua. Pia, mitheni ni gesi mbaya zaidi inayosababisha kuongezeka kwa joto ulimwenguni kuliko kaboni dioksidi – madhara yake ni mara 34 zaidi katika kipindi kinachozidi miaka 100. Karibu asilimia 24 ya gesijoto zote ulimwenguni pote hutokana na kilimo, misitu na matumizi mengine ya shamba.

Kuna njia mbalimbali ya kupunguza uchafuzi wa hewa kutoka katika chanzo hiki. Watu wanaweza kugeukia lishe linalotegemea mboga na/au kupunguza taka ya chakula, wakati huo huo wakulima wanaweza kupunguza mitheni inayotokana na mifugo kwa kutumia kikamilifu uwezo wa mifugo wa kumeng’enya chakula na kuboresha usimamizi wa maeneo ya malisho na maeneo yenye nyasi.

Taka

Kuchoma taka katika eneo lililo wazi na taka iliyozalishwa kwa uzikaji hutoa dioksini, furani, mitheni, na kaboni nyeusi zenye madhara kwenye mazingira. Ulimwenguni, inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya taka huchomwa katika eneo lililo wazi. Athari kubwa zaidi inapatikana kwenye maeneo ya mjini hususan katika nchi zinazoendelea. Zoea la kuchoma taka ya kilimo na ya manispaa hufanywa katika nchi 166 kati ya 193.

Kuboresha ukusanyaji, utenganishaji, na kutupwa kwa taka ngumu hupunguza kiwango cha taka kinachochomwa au kuzikwa. Kutenganisha taka iliyozalishwa na kuibadili kuwa mbolea au nishati kutoka kwa wanyama na mimea ambayo inaweza kutumiwa kiuendelevu, huboresha rutuba ya mchanga na huandaa chanzo mbadala cha nishati. Pia, kupunguza kadirio la thuluthi moja la chakula kinachopotezwa au kuwa taka kunaweza kuboresha hewa.

Vyanzo vingine

Si uchafuzi wote wa hewa unatokana na shughuli za binadamu. Milipuko ya kivolkaniki, dhoruba za vumbi na matukio mengine ya asili pia husababisha matatizo. Kihususa, dhoruba za mchanga na vumbi husumbua sana. Chembechembe ndogo sana za vumbi zinaweza kusafiri maelfu ya maili kwa sababu ya dhoruba hizi, chembechembe hizi pia zinaweza kubeba pathojeni na vitu vingine vinavyodhuru, na hivyo kusababisha matatizo ya mfumo wa kupumua ya muda mfupi na yaliyo tata.

تبادل آرائك، وساعدنا في نشر المعلومات عن تلوث الهواء.

التحدي

هل تحتاج إلى أدلة أو أصول عملية لتوسيم الحدث الخاص بك في يوم البيئة العالمي؟

للتحميل

كن جزءًا من الحركة العالمية وشارك الحدث الخاص بك في يوم البيئة العالمي

للتسجيل