Changamoto ya Barakoa ya Siku ya Mazingira Duniani

Tisa kati ya watu kumi hupumua hewa iliyochafuliwa. Kuanzia Mei 24, hadi #WorldEnvironmentDay (Siku ya Mazingira Duniani) tarehe 5 Juni, tunaalika kila mtu ajiunge na Shindano la Barakoa. Barakoa za uso ni ishara kuu za kuonyesha viongozi kwamba tunataka kupumua hewa safi. Kampeni ya Siku ya Mazingira Duniani inawaalika watu mashuhuri, watu wenye ushawishi, na wabunifu:

Kuamua ni hatua gani utakayochukua ili ku #BeatAirPollution (Kushinda Uchafuzi wa Hewa)

Ifuatayo ni baadhi ya mifano:

 • Kutumia usafiri wa umma au gari la pamoja, kuendesha baiskeli au kutembea
 • Kubadilisha na kutumia magari ambayo hutumia petroli na umeme au umeme tu na kuomba teksi za umeme
 • Zima injini ya gari linapokuwa limesimama
 • Punguza viwango vya nyama na bidhaa za maziwa ili kusaidia kupunguza viwango vya gesi ya mitheni unayotoa
 • Tengeneza mbolea kwa kutumia vyakula vilivyozalishwa na utumie tena vile ambavyo havijazalishwa
 • Badili ili uanze kutumia mifumo na vifaa vya kupasha moto visivyotumia nishati nyingi
 • Okoa nishati: zima taa na vifaa vya kielektroniki ikiwa havitumiki
 • Chagua rangi na mapambo yasiyo na sumu

 

 1. Fanya ahadi na uwape wengine changamoto ili wachukue hatua
  Mei 24 – Juni 4

  • Jipige picha au video ukiwa umevaa barakoa na uiweke kwenye mtandao wa kijamii. Huna barakoa

  • Kuwa mbunifu na ujitengenezee!

  • Kwenye picha au video yako elezea hatua utakayochukua ili kupunguza uchafuzi wa hewa

  • Shirikisha watu/mashirika/ kampuni 3 na uwape changamoto ya kufanya vivyo hivyo.

  • Tumia #WorldEnvironmentDay (Siku ya Mazingira Duniani) na #BeatAirPollution (Kushinda Uchafuzi wa Hewa) kwenye picha au video yako ya mtandao wa kijamii na usisahau kuongeza @UNEnvironment.

 2. Katika Siku ya Mazingira Duniani, onyesha jinsi ulivyotimiza ahadi yako!

 • Jipige picha au video nyingine ukitimiza azimio lako na uiweke kwenye mtandao wa kijamii.

 • Tumia #WorldEnvironmentDay (Siku ya Mazingira Duniani) na #BeatAirPollution (Kushinda Uchafuzi wa Hewa) kwenye picha au video zako za mtandao wa kijamii na usisahau kuongeza @UNEnvironment.