Uchafuzi wa Hewa

Hatuwezi kuacha kupumua, lakini tunaweza kufanya jambo kuhusiana na ubora wa hewa yetu

"Uchafuzi wa hewa", mada ya Siku ya Mazingira Duniani 2019, ni wito wa kuchukua hatua ya kukabiliana na changamoto kubwa zaidi ya mazingira ya wakati huu. Mada ya Siku ya Mazingira Duniani 2019, yaliyochaguliwa na Uchina mwaka huu, yanatualika sote kufikiria jinsi tunaweza kufanya mabadiliko katika maisha yetu ya kila siku ili kupunguza kiwango cha uchafuzi wa hewa tunaozalisha, na kuharibu mchango wake katika joto la ulimwengu na athari zake juu ya afya yetu wenyewe.

Takriban watu milioni 7 duniani kote hufa wakiwa wachanga kila mwaka kutokana na uchafuzi wa hewa, na vifo karibu milioni 4 hutokea Asia-Pasifiki. Watu tisa kati ya watu kumi ulimwenguni kote wako katika hatari ya viwango vya uchafuzi wa hewa ambavyo huzidi vile vinavyohesabiwa kuwa salama na Shirika la Afya Duniani.

Image removed.

Uchafuzi wa hewa hauathiri tu afya ya binadamu na ukuaji wa uchumi. Vichafuzi vingi pia husababisha joto la ulimwengu. Tazama kaboni nyeusi, ambayo hutoka kwenye injini za dizeli, kuchoma takataka na jiko chafu la kupikia. Kaboni nyeusi inaweza kusababisha mauti, lakini pia ni kichafuzi cha hali ya hewa cha muda mfupi. Ikiwa tutaweza kupunguza uzalishaji wa uchafuzi huo, tunaweza kupunguza joto la ulimwengu hadi 0.5°C katika miongo michache ijayo.

Methane, ambayo asilimia kubwa hutoka kwa kilimo, ni kichafuzi kingine. Utoaji wa methane huchangia kwenye kiwango cha ozoni ya ardhi, ambayo husababisha pumu na magonjwa mengine ya kupumua. Pia ni gesi ya joto kali zaidi ya ulimwengu kuliko dioksidi ya kaboni—athari zake ni zaidi ya mara 34 kwa kipindi cha miaka 100, kulingana na Jopo la Kimataifa la Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

Kile unachoweza kufanya

Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu inatoa fursa kwa kila mmoja wetu ili kupambana na uchafuzi wa hewa ulimwenguni kote. Na huna haja ya kusubiri hadi tarehe 5 Juni ili uchukue hatua.

Kuna vitu vingi ambavyo tunaweza kufanya: kutoka kutumia baiskeli au kutembea kwenda kazini na kurudi, kurekebisha taka yako isiyo ya kikaboni, kulazimisha mamlaka ya mitaa katika kuboresha nafasi za majani katika jiji lako. Hapa kuna mawazo mengine:

  •  Zima taa na vifaa vya eletroniki ambavyo havitumiki.
  •  Angalia kiwango cha umeme kwa mifumo ya kupikia vyakula nyumbani na meko ya kupikia ili utumie modeli inayohifadhi pesa na kulinda afya.
  • Kamwe usichome takataka, kwa sababu hatua hii inachangia katika uchafuzi wa hewa moja kwa moja.

Ni nini kingine tunachoweza kufanya ili kukabiliana na tatizo hili? Shiriki mawazo yako kwenye mtandao wa kijamii ukitumia alama #worldenvironmentday.

Endelea kuangalia hapa katika wiki zijazo kwa maelezo zaidi kuhusu kampeni ya mwaka huu, na usisahau kujisajili ili kupokea masasisho kufuatia Siku ya Mazingira Duniani 2019.