Uchina

Mwenyeji wa Ulimwenguni Pote wa Siku ya Mazingira Duniani 2019

Vidokezo Vikuu

Watu

Uchina ndilo taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu kote ulimwengu huku idadi ya watu ikiwa bilioni 1.39. Kuna makabila 56 nchini Uchina. Lugha ya kitaifa ya Uchina ni Kichina, ambayo pia  ndiyo huzungumzwa zaidi ulimwenguni. Kichina inajumuisha Kimandarini (ambayo ni maarufu zaidi) na lahaja nyingine nyingi.

Image removed.

Jiografia

Nchi ya Uchina,lenye eneo la mraba milioni 9.6, inapatikana upande wa mashariki ya Eshia, kwenye ukingo wa magharibi ya Bahari ya Pasifiki. Katika upande wa mashariki kuna Uwanda wa Tibet, unaosifiwa kama "Paa la Ulimwengu“ pamoja na kilele cha Mlima Everest ambao ni mrefu zaidi Ulimwenguni. Sehemu la kati, ambayo ina mabonde na nyanda, ina milima na misitu. Eneo la masharika limesheheni mito tambarare. Nchi ya Uchina ina mikoa 23, maeneo matano yanayojitegemea (Mongolia, Ningxia, Guangxi na Tibet), manispaa manne yanayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu (Beijing, Shanghai, Chongqing na Tianjin) na maeneo mawili maalum ya utawala (Hong Kong and Macau).

Historia

Nchi ya Uchina ni mojawapo ya nchi zenye ustaarabu kongwe na maarufu kote ulimwenguni. Kwa zaidi ya miaka 5,000, ilikua kutoka jamiii kijima hadi kuwa jamii ya kisoshialisti, na kushuhudia kua kwa dini mbalimbali na kuinuka na kusambaratika kwa ustaarabu na falme. Mwaka wa 1949, ulishihudia chanzo cha Jamuhuri ya Watu wa Uchina, ukurasa mpya umefunguliwa.

Uchumi 

Nchi ya Uchina ni nambari ya pili kote ulimwenguni na moja ya uchumi unaokua kwa kasi sana ulimwenguni, kiwango cha kua kwa pato la Nchi ni ya asilimia 6.6 mwaka wa 2018. Kilimo, viwanda vya kisasa, Teknolojia na huduma nyingine kutoka kwa sekta kuu katika uchumi. Washirika wake wakuu wa biashara ni Marekani, Japani na Korea Kusini.

Mazingira

Kuwepo kwa Mimea na wanyama bora na wengi Nchini Uchina kunatokana na hali ya hewa na georafia. Nchi ya Uchina ni makao ya panda mkubwa, Simbamarara wa Siberia, pomboo wa mto wa Yangtze, ndovu wa Eshia, tumbili, korongo wa shingo jeusi, kwarara ushungi pamoja na aina nyingine ya wanyama na ndege wasiojulikana sana.

“Nchi hii inapaswa kulinda mazingira kama mtu anavyolinda macho yake na kuchukulia mazingira kama mtu anavyochukulia maisha yake. Usasa tunaotafuta ni ule unaongozwa na wanadamu na mazingira kuishi kwa pamoja, amesema Rais wa Uchina Xi Jinping.