Siku ya Mazingira
Duniani
Mwaka wa 2022

#DUNIAMOJATU 

Kaulimbiu ya #DuniaMojaTu ni kauli iliyotumika katika Kongamano la Stockholm mwaka wa 1972, ilisisituza umuhimu wa kupatanisha wa na mazingira. Dunia inakabiliwa na majanga ya aina tatu: mazingira yanashuhudia ongezeko la joto kwa kasi mno kuliko vile watu na asili vinavyoweza kustahimili; kupoteza makazi na matashio mengine kunaweza kupelekea takriban spishi milioni 1 kuwa hatarini kuangamia; na uchafuzi unaendelea kudhuru hewa, ardhi na maji yetu.   

2022 ulikuwa mwaka muhimu kwa historia ya jamii ya mazingira duniani. Ilikuwa maadhimisho ya miaka 50 tangu kutokea kwa Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mazingira ya Binadamu Mwaka wa 1972, unachukuliwa na wengi kama mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu mazingira.  Kongamano la Stockholm lilipelekea uundaji wa wizara za mazingira na mashirika ya mazingira kote duniani na kuanzisha mikataba mingi mipya ya kimataifa ya kushirikiana kutunza mazingira. Pia huko ndiko uhusiano kati ya malengo ya kupunguza umaskini na utunzaji wa mazingira ulionyeshwa, na kupelekea kuanzishwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu.  

WALENGWA 

Jamii zilizo hatarini zaidi ulimwenguni mara nyingi ndizo huathiriwa zaidi na janga la mazingira. Kati ya watu milioni 7 wanaokufa kila mwaka kutokana na uchafuzi wa hewa, idadi kubwa ni watoto na wazee, na wengi wako katika mataifa yanayoendelea. Katika mwaka wa 2020, majanga ya tabianchi yalilazimisha watu milioni 30 kukura makwao –karibu mara tatu zaidi ya wale waliohama kutokana na vita na ghasia. Kufikia mwaka wa 2050, idadi ya watu watakaohama kutokana na changamoto za mazingira inaweza kuongezeka na kufikia kiwango cha juu cha watu milioni 200. Tunatumia kiwango sawa na 1.6 ya Dunia kudumisha maisha yetu kwa sasa, na mifumo ya ekolojia haiwezi kukimu mahitaji yetu. Kukabiliana na majanga haya ni muhimu ili kuokoa maisha na kuboresha mustakabali wa mabilioni ya watu. Watu binafsi na mashirika ya uraia ni sharti wachukue hatua muhimu za kuhamasisha na kuzihimiza serikali na sekta za kibinafsi kufanya mabadiliko makubwa.  

NCHI MWENYEJI 

Uswidi ilikuwa nchi mwenyeji wa Siku ya Mazingira Duniani mwaka wa 2022 na iliandaa Stockholm+50 kuanzia tarehe 2 to 3 mwezi Juni. Stochkolm+50 ilikuwa maadhimisho ya miaka 50 tangu kutokea kwa kongamano la kwanza la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira ya Binadamu, uliofanyika Stockholm mwaka wa 1972. Siku ya Mazingira Duniani mwaka wa 2022 ilitumia fursa hii kuonyesha baadhi ya kazi za mwanzo kabisa za Uswidi za mazingira katika kipindi cha miaka 50 iliyopita. UNEP ilishirikiana na Uswidi kuonyesha ubunifu huu kupitia mfululizo wa visa viilivyoandikwa na video fupi ambazo zilipakiwa mtandaoni. 

JIUNGE NA VUGUVUGU 

Kampeni ya #DuniaMojaTu ilitoa wito wa kushirikiana katika ngazi ya kimataifa kuleta mabadiliko chanya ili kusherehekea, kutunza na kuboresha sayari yetu. Kampeni hii pia ilitoa mifano kutoka kwa na utafiti na kukuza matendo bora, kusaidia serikali, mashirika ya biashara, taasisi na watu binafsi kuimarisha juhudi za kushughulikia mazingira, kwa kuunga mkono mabadiliko muhimu, yanayohitajika kwa dharura. Ingawa ni uamuzi wetu binafsi kufanya mabadiliko, ushirikiano wa kuchukua hatua ndio utakaobadilisha mambo. Tunahitaji kushirikiana kuleta mabadiliko ya dharura na kupelekea kuwa na Dunia endelevu zaidi na yenye haki, ambapo kila mtu anaweza kustawi.  

MAMBO MUHIMU   

Mkakati wa hali ya juu wa UNEP wa mawasiliano na mitandao ya kijamii vilizaa matunda. Kwa kutumia kaulimbiu #DuniaMojaTu, mitandao ya kijamii, video, upeperushaji wa moja kwa moja, kurasa za wavuti zinazoingiliana, matumizi ya vyombo vya habari vya jadi, na makala mafupi na marefu yaliyotolewa kama sehemu ya uhamasishaji, ushirikishwaji na kupigania hatua kuchukuliwa. Pia walifanya kazi kuangazia hafla, kampeni na kutoa matangazo ambayo yalifanyika karibu na Siku ya Mazingira Duniani.    

  • 67.5M - ni mara makala ya UNEP yalitazamwa kama vile Nambari za Juhudi Duniani, video na masasisho ya moja kwa moja, habari na hadithi.   
  • 48,540 - ni makala za habari katika nchi 166 katika lugha 54.   
  • Iluvuma na kuchukua nambari moja duniani - #SikuYaMazingiraDuniani kwa X (zamani ilijulikana kama Twitter) tarehe 5 Juni.  
  • Mwongozo wa Vitendo wa #DuniaMojaTu ulipakuliwa zaidi ya mara 55 000 – na kampeni kuweka rekodi mpya.