6 July 2020 Shughulikia binadamu, wanyama na mazingira kwa kiwango sawa ili kuzuia kutokea tena kwa janga lingine – Ripoti ya UN COVID-19 ni mfano mmoja tu wa hali ya ongezeko la magonjwa – kuanzia kwa Ebola hadi kwa MERS, homa ya West Nile na homa ya Bonde la Ufa – husababishwa na virusi kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu. Utatiti mpya unatoa mapendekezo kumi, na kuainisha Afya Moja (One Health) kama njia mwafaka ya ya kuzuia na kukuabiliana na majanga katika siku zijazo.  Ongezeko la magonjwa kotoka kwa wanyama husababishwa na uharibifu wa mazingira yetu halisia - kupitia uharibifu wa ardhi, matumizi mabaya ya wanyamapori, uchimbaji wa mali ghali, mabadiliko ya tabianchi na changamoto zinginezo.
 • COVID-19 ni mfano mmoja tu wa hali ya ongezeko la magonjwa – kuanzia kwa Ebola hadi kwa MERS, homa ya West Nile na homa ya Bonde la Ufa – husababishwa na virusi kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu.
 • Utatiti mpya unatoa mapendekezo kumi, na kuainisha Afya Moja (One Health) kama njia mwafaka ya ya kuzuia na kukuabiliana na majanga katika siku zijazo. 
 • Ongezeko la magonjwa kotoka kwa wanyama husababishwa na uharibifu wa mazingira yetu halisia - kupitia uharibifu wa ardhi, matumizi mabaya ya wanyamapori, uchimbaji wa mali ghali, mabadiliko ya tabianchi na changamoto zinginezo.

 

Nairobi, Julai 06, 2020 – Janga la COVID-19 linapoendelea kusababisha vifo na kuathiri uchumi kote duniani, ripoti mpya yaonya kuwa mikurupuko zaidi itatokea iwapo serikali hazitachukua hatua madhubuti kuzuia wanyama kuambukiza binadamu magonjwa zaidi kutoka kwa wanyama. Pia, imetoa mapendekezo kumi ya kuzuia ugonjwa tandavu kutokea siku zijazo.

Ripoti, Kuzuia ugonjwa mtandavu kutokea tena: Magonjwa kutoka kwa wanyama na jinsi ya kuyazuia kuenea sana ni mradi unaotokana na ushirikiano wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI).

Unabainisha mienendo saba inayopelekea kuongezeka kwa magonjwa yanayotoka kwa wanyama, ikiwa ni pamoja na ongezeko la hitaji la protini kutoka kwa wanyama; ongezeko la kilimo kwa njia zisizostahili, ongezeko la matumizi mabaya ya wanyamapori; na janga la mabadiliko ya tabianchi. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa haswa Afrika, ambayo imekumbwa na kukabiliana na majanga kadhaa ya magonjwa kutoka kwa wanyama, ikijumuisha mikurupuko ya Ebola iliyotokea hivi karibuni, inaweza kutoa mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na mikurupuko katika siku zijazo.

"Sayansi inaonyesha wazi kuwa iwapo tutaendelea kutumia vibaya wanyamapori na kuendelea kuharibu mifumo ya ekolojia, tutaendelea kushuhudia ongezeko kwa aina hii ya magonjwa yanayoenea kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu katika miaka ijayo," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP Inger Andersen. Magonjwa tandavu ni tishio kwa maisha na kwa uchumi, na jinsi ambavyo tumeona katika miezi kadhaa iliyopita, Wanaoathirika zaidi ni watu maskini kabisa na walio hatarini zaidi. Ili kuzuia mikurupuko katika siku zijazo, ni shariti tujitolee kwa dhati kutunza mazingira yetu."

“zoonotic disease” au “zoonosis” ni ugonjwa unaoenezwa kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu. COVID-19, ambayo tayari imesababisha vifo vya watu zaidi ya nusu bilioni kote duniani, kuna uwezekano mkubwa kuwa ilitoka kwa popo. Ila COVID-19, ni mojawapo tu ya ongezeko la magonjwa yaliyotokea hivi karibuni ikiwa ni pamoja na Ebola, MERS, homa ya West Nile na homa ya Bonde la Ufa – ambayo kuenea kwake kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu huchangiwa na shinikizo la kiantropojeniki.

Kila mwaka, watu wapatao milioni mbili, hasa kutoka kwa nchi za uchumi wa chini na nchi za uchumi wa kati, hufariki kutokana na magonjwa yaliyopuuzwa yanayotoka kwa wanyama. Mikurupuko hiyo inaweza kusababisha magonjwa sugu, vifo, kupungua kwa mifugo katika nchi zinazoendelea, sababu kuu inayochangia mamiliani ya wakulima wadogowadogo kuendelea kuishi katika umaskini uliokidhiri. Kwa kipindi cha karne mbili tu iliyopita, magonjwa kutoka kwa wanyama yamesababishia uchumi hasara ya zaidi ya dola bilioni 100, bila kujumuisha gharama za ugonjwa mtandavu wa COVID-19 inayotarajiwa kufikia dola zaidi ya trilioni 9 kwa kipindi cha miaka michache ijayo.

Nchi za Afrika zina uwezo wa kuwa mstari mbele katika juhudi za kukabiliana na magonjwa tandavu

Magonjwa kutoka kwa wanyama yanaendelea kuongezeka kote duniani, na nchi za Kiafrika - baadhi ya nchi hizo zikiwa zimefaulu kukabiliana na mikurupuko sugu ya magonjwa kutoka kwa wanyama - zina uwezo wa kukabiliana na mikurupuko katika siku zijazo kwa kutumia mbinu zinazojali binadamu, wanyama na mazingira. Bara hili ni makao kwa misitu mikubwa duniani inaysababisha mvua na ardhi nyingine ambayo ni makaazi ya wanyamapori. Afrika pia ni makaazi kwa idadi ya watu inayoendelea kukua kwa kasi, inayopelekea ongezeko la mtagusano kati wa mifugo na wanyamapori, hali inyochangia hatari ya kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyama.

"Hali barani kwa sasa ni mwafaka kwa kuimarisha juhudi za kukabiliana na magonjwa yaliopo yanayotoka kwa wanyama na kuzuia kuzuka kwa magonjwa mapya," alisema Mkurugenzi Mkuu wa ILRI Jimmy Smith. "Kwa kuweza kukabiliana na Ebola na magonjwa mengine yanayozuka, nchi za Kiafrika zinaonyesha uwezo wake wa kukabiliana na mikurupuko. Kwa mfano, kwa kutumia, mbinu mpya za majaribio badala ya kutumia sheria zilizowekwa kukabiliana na magonjwa, ambazo ni mwafaka kwa maeneo yaliyo na rasilimali kidogo, na zinaleta pamoja watu, wanyama na wataalamu wa mazingira waounga mkono mradi wa One Health.

Waandishi wa ripoti hiyo wanapendekeza mbinu ya One Health --inayoleta pamoja wataalamu wa afya ya umma, madaktari wa mifugo na wataalamu wa mazingira -- kama njia mwafaka ya kuzuia na kukabiliana na magonjwa kutoka kwa wanyama na magonjwa tandavu.

Mapendekezo 10

Ripoti hiyo inaanisha hatua kumi zinazoweza kufuatwa na serikali kuzuia mikurupuko ya magonjwa kutoka kwa wanyama siku zijazo:

 • Kutumia njia inayojumuisha sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na One Health;
 • Kuimarisha utafiti wa kisayansi kuhusiana na magonjwa kutoka kwa wanyama;
 • Kutumia mbinu zisizokuwa na gharama ghali wakati wa kutathmini madhara ya magonjwa katika jamii;
 • Kuhamasisha kuhusu magonjwa kutoka kwa wanyama;
 • Kuimarisha ufuatiliaji na kudhibiti mienendo inayosababisha kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyama, ikijumuisha mifumo ya chakula;
 • Kutuza wanaokuza mashamba kwa njia endelevu na kubuni njia mbadala za kuhakikisha kuwa kuna chakula cha kutosha bila kuharibu maeneo ya makaazi na bayoanuai;
 • Kuboresha utunzaji wa mimea na wanyama dhidi ya magonjwa, kutambua kinachosababisha kuzuka kwa magonjwa wakati wa ufugaji na kuhimiza matumizi ya hatua zilizodhibitishwa ili kukabiliana na magonjwa kutoka kwa wanyama.
 • Kuunga mkono matumizi endelevu ya mandhari na maeneo ya bahari ili kuwezesha ukulima unaojali wanyamapori.
 • Kuimarisha uwezo wa wadau katika sekta ya afya katika nchi zote;
 • Kufanyia kazi mbinu ya One Health wakati wa matumizi ya ardhi na kupanga, kutekeleza na kufuatilia maendeleo na matumizi mengine ya ardhi kwa njia endelevu.

Uzinduzi wa ripoti hii unatokea Siku ya Magonjwa Kutoka kwa Wanyama Duniani Mnamo Julai mwezi wa 6 mwaka wa 1885, Pasteur alifaulu kutoa chanjo ya kwanza dhidi ya kichaa cha mbwa, ugonjwa kutoka kwa wanyama.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP):

UNEP in mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.    

Kuhusu Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo

Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) ni Shirika lisilo la biashara linalosaidia watu kutoka kwa nchi za kipato cha chini na kipato cha kati kuboresha maisha yao, kuongeza kipato chao na kuboresha mashamba yao kupitia wanyama ambao wanasalia kuwa nguzo ya wakulima wadogowadogo na kwa kampuni katika nchi zote zinazoendelea. ILRI ni kituo cha utafiti cha CGIAR makao makuu yakiwa Kenya na Ethiopia na kina ofisi zingine 14 barani Afrika na Asia.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP, +254717080753, [email protected]

David Aronson, Media na Ushughulikiaji wa Sera, ILRI, [email protected]

 

covid-19 response logo

Recent Stories

Kuanzia nchi zinazoweka sera hadi kwa wahamasishaji wa #TutunzeMazingira, hatua kubwa zilipigwa mwaka wa 2020 zilizoonyesha huduma kuu…