mobile header
7 March 2019 Kampeni ya hewa safi ulimwenguni inavyozidi kushika kasi, IKEA imezindua pazia ya kusafisha hewa

Tunapozungumzia uchafuzi wa hewa, huenda taswira unayopata kwanza ni ya maghorofa yaliyofunikwa na mchanganyiko wa ukungu na moshi, moshi palipo msongamano wa magari na dohani zinazotoa moshi mwingi, lakini utafiti mpya umefumbua sumu zisizoonekana zinazochafua hewa nyumbani kwetu.

Hadithi

Tunapozungumzia uchafuzi wa hewa, huenda taswira unayopata kwanza ni ya maghorofa yaliyofunikwa na mchanganyiko wa ukungu na moshi, moshi palipo msongamano wa magari na dohani zinazotoa moshi mwingi, lakini utafiti mpya umefumbua sumu zisizoonekana zinazochafua hewa nyumbani kwetu.

Tunapozungumzia uchafuzi wa hewa, huenda taswira unayopata kwanza ni ya maghorofa yaliyofunikwa na mchanganyiko wa ukungu na moshi, moshi palipo msongamano wa magari na dohani zinazotoa moshi mwingi, lakini utafiti mpya umefumbua sumu zisizoonekana zinazochafua hewa nyumbani kwetu.

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Colorado Boulder wamegundua kuwa kupika, kusafisha na shughuli zingine za kawaida za nyumbani zinaweza kuzalisha viwango vikubwa vya kemikali fushi na za chembechembe ndani ya nyumba hivyo kufanya kiwango cha uchafuzi wa hewa mle nyumbani kuwa sawa na kile cha miji iliyochafuliwa.

Marina Vance, Profesa Msaidizi wa uhandisi mitambo kwenye Chuo Kikuu cha Colorado Boulder, aliongoza timu iliyotumia sensa na kamera mahiri zaidi kupima kwa mwezi mmoja viwango vya uchafuzi wa hewa katika nyumba iliyoundwa. Matokeo ya mwisho yanasubiriwa lakini walichogundua ni kuwa shughuli za msingi kama vile kuchemsha maji, kunachangia uchafuzi wa hewa kwa kiasi kikubwa.

Uchafuzi wa hewa, umetajwa kuwa hatari kubwa zaidi kwa mazingira, unasababisha vifo vya takribani watu milioni 7 kila mwaka, huku watu 9 kati ya 10 ulimwenguni kote wanapumua hewa chafu. Jamii maskini zaidi ndizo zinaoathirika zaidi. Thuluthi moja ya vifo vinavyosababishwa na kiharusi, saratani ya mapafu na magonjwa ya moyo husababishwa na uchafuzi wa hewa.

Uchafuzi wa hewa nyumbani husababisha vifo vya karibu watu milioni 4 kila mwaka, hasa katika katika nchi zinazoendelea barani Asia na Afrika ambako teknolojia na fueli zinazochafua hewa, zikiwemo taa za kerosini na moto unaowashwa nje, hutumika kupika, kupashajoto na kumulika.

Kutokana na watu zaidi kuendelea kuhamasishwa katika nchi zinazoendelea, mbinu tofauti tofauti kuanzia visafishaji hewa hadi mimea inayopandwa ndani ya nyumba zimependekezwa ili zitumike kuchuja chembechembe hatari nyumbani mwetu

image
Kitambaa cha GUNRID. Picha imepigwa na Inter IKEA Systems B.V. 2016

Sasa, kampuni ya Uswidi ya kuunda samani IKEA imetengeneza pazia ambayo kwa mujibu wake inasafisha hewa kwa kutumia teknolojia inayoweza kuzalishwa kwa njia zingine katika nyumba. Sehemu ya nje imeundwa kwa kutumia madini hivyo kuwezesha pazia ya GUNRID kuyeyusha kemikali zilizo kwenye hewa inapofikiwa na mwangaza wa jua au ndani ya nyumba. Mchakato huu ni sawa na usanidinuru.

“Mojawapo ya malengo yetu ni kusafisha hewa, ambapo tumelenga kupunguza kabisa kemikali kwenye hewa na kuwawezesha watu kusafisha

hewa nyumbani mwao, kufikia mwaka wa 2030,” alisema Lena Pripp-Kovac, mkuu wa udumishaji kwenye kampuni ya Inter IKEA Group.

“Pazia ya GUNRID ya kusafisha hewa ni hatua moja ya safari hii. Tulitaka kubuni njia ya kusafisha hewa isiyochukua nafasi kubwa katika nyumba na iliyo rahisi kutumia, itakayofaa na ya bei nafuu, hivyo tukajadiliana: je, inawezekana kutumia nguo kusafisha hewa? Kando na kuwawezesha watu kupumua hewa safi nyumbani, tunatarajia kuwa GUNRID itasaidia katika kuwahamasisha kuhusu uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba, hivyo kuchochea mitindo inayochangia hewa safi ulimwenguni,” aliongezea.

Teknolojia ya GUNRID iliundwa na IKEA, kwa ushirikiano na vyuo vikuu barani Ulaya na Asia, na wasambazaji na wavumbuzi. Wana matumaini kuwa teknolojia hii itatumika baadaye kwa nguo nyingine.

“Kama kampuni ya fanicha za nyumbani, tuona kuwa tuna fursa maalum kutathmini pia kwa njia tofauti changamoto zinazohusiana na kemikali zinazochafua hewa,” alisema Pripp-Kovac.

Uvumbuzi na mikakati hii bunifu itajadiliwa kwa kina kwenye kikao cha nne cha idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa kitakachofanyika mwezi wa Machi nchini Kenya. Wito wa kikao hiki kupanua mawazo na kuishi kwa uwajibikaji. Akiandika kwenye Ripoti ya Mwaka wa 2018 ya idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa kabla ya kikao kijacho, kaimu Mkurugenzi Mtendaji Joyce Msuya ameeleza kuhusu mikakati iliyowekwa kukabiliana na uchafuzi wa hewa.

“Pia tumeshirikiana na Shirika la Afya Ulimwenguni kuandaa mkutano wa kwanza kabisa ulimwenguni kuhusu uchafuzi wa hewa, unasababisha vifo vya

mamilioni ya watu kila mwaka, na tunaendelea kuunga mkono mikakati na sera za kitaifa kuhusu usafiri safi,” alisema.

Idara ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa imeshirikiana na Climate and Clean Air Coalition na Shirika la Afya Ulimwenguni kuendesha kampeni ya Breathe Life kote ulimwenguni ili kuhamasisha na kuunga mkono mipango ya hewa safi zaidi.

image
Sampuli kifani ya GUNRID pazia inayosafisha hewa. Picha imepigwa na Inter IKEA Systems B.V. 2016.

Huku wengi wakisifia uvumbuzi wa IKEA, baadhi ya wakosoaji wamesema kuwa sharti ijizatiti zaidi kupunguza uchafuzi kutokana na utengenezaji. IKEA imesema kuwa kwa miaka mingi sasa imekuwa ikishughulikia hili kwa kuondoa kemikali hatari na kupunguza uchafuzi wa hewa.

“GUNRID ni mfano tu mmoja wa hatua zote tunazochukua ili kuchangia katika kusafisha hewa,” alisema Pripp-Kovac, akitaja kuwa IKEA haitumii tena kemikali zinazoaminika kuwa hatari au zinazosababisha mzio, ikijumuisha gesi ya maji ya kidhuru bakteria. Alisema pia kuwa kampuni kubwa zaidi iliyopewa haki maalum na IKEA, INGKA Group, inalenga kutochafua hewa kabisa kutokana na usafirishaji wa bidhaa za nyumbani kufikia mwaka wa 2025.

Mwezi uliopita wa Novemba, IKEA pia ilizindua Better Air Now! Mpango wa kutumia majani makavu ya mchele, ambayo kawaida hutupwa na kuchomwa baada ya kuvuna mchele, kuwa malighafi ya kutengeneza bidhaa upya. IKEA imejitolea kuhifadhi mazingira dhidi ya uchafuzi wa hewa kwa kulenga kutumia tu nishati mbadala katika utendakazi wake, na kwa kukuza uzalishaji wa nishati mbadala.

“Tunafahamu kuwa hakuna mwafaka mmoja wa kutatua tatizo la uchafuzi wa hewa,” alisema Pripp-Kova. “Pia tunafahamu kuwa ni muhimu kuzungumzia na kuwashawishi watu kuvumbua mbinu mpya zitakazoleta suluhu.”

Recent Stories
Habari kwa vyombo vya habari

Nairobi, tarehe 15 Machi 2019 – Hivi leo, kiongozi wa uwakilishi wa China, Zhao Yingmin, naibu wa waziri wa mazingira na Joyce Msuya, kaimu wa…

Habari kwa vyombo vya habari

Zaidi ya miaka 20 baada ya Beijing kuanza kutafuta njia za kuboresha…