mobile header
28 January 2019 Kubadilisha dizeli kuwa wino nchini India

Tangu Arpit Dhupar, mwanzilishi wa Chakr Innovation, ashinde tuzo la Young Champions of the Earth ya Asia na maeneo ya Pacific, uliokuwa mwanzo wake, amejiendeleza sana.

Hadithi

Tangu Arpit Dhupar, mwanzilishi wa Chakr Innovation, ashinde tuzo la Young Champions of the Earth ya Asia na maeneo ya Pacific, uliokuwa mwanzo wake, amejiendeleza sana. Chakr Innovation inaokota chembembe zinazochafua mazingira zinazotoka kwa injini zinazotumia dizeli.

Tangu  Arpit Dhupar, mwanzilishi wa Chakr Innovation, ashinde tuzo la Young Champions of the Earth prize for Asia na maeneo ya Pacific, uliokuwa mwanzo wake, amejiendeleza sana. Chakr Innovation inaokota chembembe zinachafua mazingira zinazotoka kwa injini zinazotumia dizeli na kuifanya wino.

Jenereta zinazotumia dizeli zinatumiwa sana India nguvu za umeme zinapopotea, na zinatoa dizeli ambao haijachomeka au moshi. Katika sehemu hambako hakuna nguvu za umeme, jenereta zinazotumia dizeli ndizo hutumiwa kama chanzo cha msingi cha nishati na zinatumiwa kwa takriban masaa nane kwa siku.

Chakr Innovation inataka kuondoa kiwango cha uchafuzi wa hewa katika Delhi, ambao unachangiwa zaidi na uchafu unaotolewa na jenereta za dizeli. Uchafu kama huo unapelekea wiani wa chembembe hizi za kiwango cha juu kama mikrogramu 300 kwa kila mita ya ujazo. Katika viwango kama hivyo, moshi inakuwa hatari kwa afya ya binadamu: kulingana na usalama wa World Health Organization uchafu huu haufai kupita mikrogramu 23 kwa kila mita ya ujazo.

“Moshi tunaonasa ni laini na nyepesi sana na hivyo haiwezi ikachungwa na mapua yako ama mapafu na hivyo basi inaenda kwenye damu,”Dhupar alisema.

“Hii ni hatari kwa afya ya binadamu.Tumeunda teknolojia inayookota chembechembe hizo za moshi kabla zifike kwenye anga ili zisisababishe athari hasi kwa utendakazi wa injini. Jambo hili halijawahi fanyika katika sekta hii.”

Kupiga chapa kwa kutumia uchafuzi, Chakr Innovation inatengeneza wino kutokana na moshi.Kifaa cha kampuni hii kinachoitwa Chakr Shield, kinaokota chembechembe za moshi kwa kuzifanya ziwe katika hali ya kioevu, ikizuia chembechembe hizi ndogo za moshi kubembwa tena na hewa.

Pindi tu chembechembe hizi za moshi, chuma nzito na vitu hatari vinapotenganishwa, rangi inatolewa na kiunganishi kinaongezwa ili kuundwa wino.

Image removed.

Image removed.
Kuchora na uchafuzi na kubadilisha moshi na kuwa wino. Picha imepigwa na: Chakr Shield

Kampuni hii  imeuza Zaidi ya vifaa 60 ikiwa na viwanda 18 kama wateja wao.Uwekaji wa kwanza wa vifaa hivi ulifanywa katika American Tower Corporation na ule mkubwa zaidi ukiwa wa  kampuni za mafuta na gesi ambapo tatizo kuu lilikuwa kukiweka kifaa juu ya maghorofa marefu.

Mteja mwingine wa Chakr ni Dell – ambayo inatumia wino unayotokana na moshi kuchapisha maandishi katika masanduku – hatua ndogo katika kupunguza mamilioni ya vifo vinavyotokana na uchafuzi kila mwaka. Tata Group ni shirika lingine kubwa linalotumia teknolojia ya Chakr ili kupunguza uchafuzi wa mazingira kutoka kwa upande wao.

“Wino ni bidhaa nzuri na ya maana lakini si tatizo pekee tunayolenga kutatua.Hakuna upungufu wa wino duniani. Tatizo tunayotatua ni kupunguza uchafuzi: hii ndio uti wa mgongo wa biashara yetu”, Dhupar anaelezea.

“Moshi ni nyepesi sana na ni ndogo mara 1000 kuliko kipenyo cha nywele,” aliongezea.Kaboni tunayookota inachukua sehemu kubwa na inaweza ikatumika katika kusafisha maji.Hivyo basi, tutakuwa tunatumia uchafuzi wa hewa kutatua uchafuzi wa maji! Lakini majaribio haya bado yako katika hatua zake za mwanzo.”

“Sisi ni kampuni ya uvumbuzi na si ya uzalishaji. Katika siku za usoni, tunafanya kazi kaatika uvumbuzi wa kushughulikia uchafuzi wa hewa kutoka kwa madohani, vifaa vya kuchemshia, vifaa vya kuchoma takataka na meli – hivyo basi tunahitajika kuendelea kuvumbua.”

Tunahimiza kila mtu anayetaka kuleta tufauti nkatika sayari yetu kuangalia kama wana kinacho hitajika ili kuwa Young Champion wa dunia.Angalia mtandao huu mara kwa mara – nafasi ya kuwasilisha ombi itafunguliwa hivi karibuni! Young Champions of the Earth Prize imewezeshwa na Covestro.

Recent Stories
Habari kwa vyombo vya habari

Nairobi, tarehe 15 Machi 2019 – Hivi leo, kiongozi wa uwakilishi wa China, Zhao Yingmin, naibu wa waziri wa mazingira na Joyce Msuya, kaimu wa…

Habari kwa vyombo vya habari

Zaidi ya miaka 20 baada ya Beijing kuanza kutafuta njia za kuboresha…