mobile header
18 January 2019 Kujiunganisha tena na mazingira bora na bado dhaifu

Mahojiano na Silvia Calvó, Waziri wa Mazingira, Kilimo na Ustawi wa Andora 

Mahojiano na Silvia Calvó, Waziri wa Mazingira, Kilimo na Ustawi wa Andora 

Hadithi

Mahojiano na Silvia Calvó, Waziri wa Mazingira, Kilimo na Ustawi wa Andora 

Je, ni suala lipi unalodhani kuwa ndilo kuu leo na ni kwa nini?

Ninadhani kuwa tatizo kuu la kimazingira tunalokumbana nalo sasa ni utumiaji mbaya na usio wa ustawi wa rasilimali za asili wa binadamu. Hii inachangia uchafuaji wa maji na hewa, mabadiliko ya hewa, upungufu wa viumbe hai na masuala mengine yote ya mazingira yaliyoshuhudiwa katika miongo ya hivi karibuni.

Tatizo hili labda ni kutokana na ukweli kuwa wanadamu wametenganishwa kabisa na uhusiano wao na asili, wakichukulia kimakosa kuwa, kwa usaidizi wa teknolojia, tunaweza kujiweka huru kutokana na mipaka ambayo asili hutuwekea. Andora, nchi ya milima ya chini ya 500 km2, ina mazingira kwasi na yaliyo dhaifu. Hukaribisha watalii milioni nane kwa mwaka, hivyo ni lazima tuwe macho sana kwa shinikizo tunaloweza kuzipa rasilimali zetu za asili.

Je, ni zipi unazodhani kuwa njia za utendaji za kushughulikia suala hili?

Sisi tunaoishi katika nchi zilizokua zaidi labda tunapaswa kutoa sehemu ya jinsi tunavyoishi kwa kuzingatia utumiaji wa fueli za kitambo (kwa usafiri, kupasha joto na hali ya hewa), utumiaji wa chakula (kuhusiana na nyama nyingi zaidi katika chakula chetu na utupaji chakula) na mambo mengine ya aina hii. Hii inawezakuwa na athari ya moja kwa moja sana kwa matumizi yetu na ingeanzisha kile kiitwacho "uchumi wa rangi ya manjano", ambao hujumuisha kila kitu kutoka kwa kanuni za uchumi wa mviringo hadi utengenezaji wa nishati safi.

Ingekuwa jambo la muhimu sana kwa nchi ambazo hazijapata maendeleo ya aina hii, ambayo ni kali sana kwa asili, kutimiza maendeleo ya kiwango sawa bila kupitia hatua zote zinazojulikana kuwa na athari mbaya kwa mazingira na kwa afya ya watu. Hii ingehusisha maedeleo ya moja kwa moja ya mifano ya jamii ambayo hutumia rasilimali chache, ikileta ahadi ya kujitolea ya uhamaji endelevu, nishati zinazoweza kutumiwa tena na utumiaji kwa njia ya uwajibikaji zaidi, katika lengo la kuongeza jamii bunifu za kimfano ambazo wanachama wake hakika watakumbana na matatizo machache ya afya.

image

Ni vipi unavyoweza kuhimiza umma kuunga mkono mafundisho ya kimazingira?

Ili kufikia mabadiliko ya mfano ni muhimu kuungwa mkono na jamii kwa jumla kwa njia ya kufanya kazi inayoheshimu mazingira. Watu wanapaswa kuarifiwa kwa njia sahihi, wanahitaji suluhu za ubunifu na zinazofikika, na huenda wakahitajika kutia bidii iwapo wataenda kinyume na mfano wa kuvutia unaotawala wa utumiaji.  Nina uhakika kuwa mabadiliko yatafanyika kwa kizazi kipya na kuwa ni wao tunaopaswa kufanya kazi nao. Nchini Andora, karibu asilimia 70 ya watoto wetu wanaosoma na vijana huudhuria shule za kijani kibichi, ambazo zimepangwa kukumbana na changamoto mpya na dhamana za ustawi, kwa njia zozote na kwa nyanja zote za maisha ya shuleni.

Zaidi ya yote, tunapaswa kutambua dhamana kuu ya huduma za mfumo wa ikolojia unaotolewa kwetu na viumbe hai, na tunapaswa kurejesha tena heshima iliyo muhimu kwa asili iwapo wanadamu watatambua tena nafasi waliyo nayo duniani kwetu. Andora ni nchi ya milima ambapo sehemu kubwa ya watu huishi karibu na milima. Ili jamii yetu iweze kurejesha tena uhusiano wake na asili, tunajenga mfumo wa njia za rangi ya kijani kibichi unaounganisha maeneo ya mjini na sehemu zilizolindwa, ikiwaruhusu wananchi, familia na watu waliozeeka kufurahia mandhari yetu ya asili na ya mashambani kwa usalama kamili.

Recent Stories
Habari kwa vyombo vya habari

Nairobi, tarehe 15 Machi 2019 – Hivi leo, kiongozi wa uwakilishi wa China, Zhao Yingmin, naibu wa waziri wa mazingira na Joyce Msuya, kaimu wa…

Habari kwa vyombo vya habari

Zaidi ya miaka 20 baada ya Beijing kuanza kutafuta njia za kuboresha…