mobile header
4 March 2019 Shirika La Umoja Wa Mataifa limetoa Ripoti Ya Kila Mwaka

Siku ya leo shirika la Mazingira ya Umoja wa Mataifa limetoa ripoti yake ya Kila mwaka ya mwaka wa 2018, inayobainisha kazi ya shirika hili kuhusu masuala kuanzia kupigana na uchafuzi wa hewa na bahari hadi kusaidia mataifa kufikia malengo yao ya kupunguza gesi zinazochafua mazingira.

Hadithi

Siku ya leo shirika la Mazingira ya Umoja wa Mataifa limetoa ripoti yake ya Kila mwaka ya mwaka wa 2018, inayobainisha kazi ya shirika hili kuhusu masuala kuanzia kupigana na uchafuzi wa hewa na bahari hadi kusaidia mataifa kufikia malengo yao ya kupunguza gesi zinazochafua mazingira.

“Licha kuwa na changamoto nyingi mwaka wa 2018, tuliona matumaini katika juhudi na kujitolea kote ulimwenguni katika kutumia mbinu mpya ya kufanya biashara zinazokabiliana na matatizo ya kimazingira tunayokumbana nayo,”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mataifa Joyce Msuya. “Jukumu letu katika kubainisha mbinu bora zaidi, kutetea na kuleta serikali mbalimbali, chama cha raia na biashara pamoja lilionekana kuwa muhimu tena.”

Ripoti, iliyotolewa mtandaoni kabla ya Mkutano wa Baraza  la mazingira ya Umoja wa Mataifa, inaonesha kuwa kasi ya kuchukua hatua kuhusu masuala mengine ya kimazingira yanayohusiana inaongezeka.

Siku ya Mazingira kote Ulimwenguni 2018 ilichochea hatua ya kukabili uchafuzi mazingira kwa palastiki, kwa kufikia mamia ya mamilioni ya watu katika zaidi ya nchi 190 huku nchi ya India ikiahidi kukomesha matumizi ya plastiki zinazotumiwa mara moja kufikia 2022.

Shirika la Mazingira ya Umoja wa Mataifa limeshirikiana na Shirika la Afya Duniani kupanga mkutano wa kwanza kabisa ulimwenguni kote kuhusu uchafuzi wa hewa, unaowaua mamilioni ya watu kila mwaka na kuunga mataifa mikono kuboresha hewa kupitia kutumia magari yanayotumia umeme, ufaafu katika kutumia mafuta na juhudi nyingine zaidi.

Mashirika na nchi - zilizokutanishwa na Shirika la Mazingira ya Umoja wa mataifa - ziliungana kuokoa Cuvette Central Peatlands katika Bonde la Kongo, ambayo ni makaazi ya aina 14 ya miti na wanyama wanaohatarishwa na inahifadhi kaboni inayotoshana na uchafuzi wa mazingira kwa gesi miaka tatu.

Ripoti hii inaonesha mchango wa Shirika la Mazingira ya Umoja wa mataifa  katika sehemu nyingine zaidi, ikiwemo kuunda kiwanda cha kuunda vifaa vya kupasha ubaridi kutoathiri hali ya anga, kusaidia jumuiya katika eneo la Darfur kupunguza migogoro ya rasailimali hali anga inapobadilika na kufunza walinda usalama ili waweze kutekeleza sheria za kimazingira kwa njia bora zaidi.

Ripoti ya mtandaoni pia itaakisiana na Ripoti ya Utekelezaji wa Mpango, ukaguzi tambullizi wa mpango wa kazi unoakubalika na Nchi Wanachama.

“Shirika la Mazingira ya Umoja wa Mataifa limekuwa na litaendelea kuwa mtendaji muhimu katika kuunga mataifa mbalimbali mkono kutimiza ahadi zao,” alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa- António Guterres.
 

Kupata maelezo zaidi, tafadhali soma, Ripoti ya kila Mwaka ya 2018.

Recent Stories
Habari kwa vyombo vya habari

Nairobi, tarehe 15 Machi 2019 – Hivi leo, kiongozi wa uwakilishi wa China, Zhao Yingmin, naibu wa waziri wa mazingira na Joyce Msuya, kaimu wa…

Habari kwa vyombo vya habari

Zaidi ya miaka 20 baada ya Beijing kuanza kutafuta njia za kuboresha…