Bayoanuai

Bayoanuai ni nguzo ya maisha duniani na nguzo ya maendeleo yanayofanywa na binadamu.

Bayoanuai—aina mbalimbali ya viumbe katika makaazi yoyote yale, ikujumuisha wanyama wakubwawakubwa, mimea, vimelea na viumbe wadogowadogo—iko hatarini zaidi kushinda kipindi kingine chochote kwenye historia. Wakati wa Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka wa 2020 wito unatolewa wa kuchukua hatua za dharura za kutunza bayoanuai. 

Kauli mbiu ya Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka wa 2020—iliyokubaliwa bila kupingwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Colombia, mwenyeji wa mwaka huu—inatoa wito kwetu sote kuchunguza jinsi tunavyoweza kubadili jinsi tunavyoishi ili kutilia maanani suala la kuboresha mazingira na kukabiliana na uharibifu wa bayoanuai. 

Flickr/CIAT
Flickr/CIAT

Viumbe vingi viko karibu kuangamia, huku aina milioni 1 ya mimea na wanyama wakiwa hatarini zaidi. Tunaendelea kupoteza aina ya viumbe karabu zaidi ya mara 1000 zaidi ya hali ya kawaida. Hali hii imepelekea wanasayansi kudai kuwa tunaelekea awamu ya sita ya kuangamia kwa viumbe kwa idadi kubwa zaidi. Kwa wastani, wanyapori wawepungua kwa zaidi ya mara 60 kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita. Kwa kuzingatia hali hii, aina ya viumbe inapungua kwa mamia haraka zaidi kuliko kasi ya wastani iiyoshuhudiwa katika kipindi cha miaka milioni kumi iliyopita.

Inawezekana kuboresha mazingira. Ni kwa kuelewa tu umuhimu wa mazingira kwa maisha yetu na kwa ubora wa kiwango cha maisha yetu ndipo tunaweza kupata manufaa yake kikamilifu.

Mwaka wa 2020 ni muhimu wa kufanya maamuzi kwa manufaa ya sayari na kwa manufaa ya watu. Pia, ni muhimu kwa viumbe wote duniani. Ijapokuwa mwaka wa 2020 pia unahitimisha Karne ya Bayoanuai ya Shirika la Mazingira la Umoja, wanasayansi wanaendelea kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuitahadharisha kuhusu kuharibika kwa bayoanuai. Kuishi vyema na mazingira—ni lengo lililowekwa na viongozi duniani kufifikiwa kufikia mwaka wa 2050—lengo hili haliwezi kufikiwa tusipokomesha kuharibika kwa bayoanuai katika sayari yetu kufikia mwaka wa 2030.

Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka huu ni muhimu ili kuhamasisha kuhusu bayoanuai na jinsi kuitunza ni muhimu kwa maisha ya viumbe wote duniani, na ni juhudi ya kufanya mazingira kuwa kitovu cha uamuzi wote wakati wa Kongomano la Wanachama wa Mkataba wa Bayoanwai ya Kibayolojia utakaotokea Kunming nchini Uchina mwezi wa Oktoba.

Ni kipi unachoweza kufanya

Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka huu inatoa fursa kwa kila mmoja wetu—watu binafsi, mashirika, makampuni ya kibinafsi na serikali—ya kuchukua hatua za kukabiliana na uharibifu wa bayoanuai. Na si lazima usubiri hadi tarehe 5 mwezi wa Juni ili kuchukua hatua—kuna shughuli zilizowekwa kwa siku maalum kadhaa kabla ya Siku ya Mazingira Duniani:

Kuna vitu vingi mno tunavyoweza kufanya: kuanzia kutumia na kuzalisha bidhaa kwa njia endelevu hadi kupunguza aina ya viumbe hatari na kushinikiza serikali kuboresha miji ili kutochafua mazingira. Hapa kuna mambo zaidi:

  • Nunua bidhaa zisizodhuru mifumo ya ekolojia
  • Tumia chakula kisicho na kemikali nyingi
  • Usitupe taka ovyoovyo

Je, ni nini kingine tunachoweza kufanya kukabiliana na hali hii. Shiriki mawazo yako kwa mitandao ya kijamii ukitumia hashitagi#SikuYaMazingiraDuniani.

Tembelea ukrasa huu majumaa yajayo ili kupokea ujumbe zaidi kuhusu kapeni za mwaka huu na usisahau kujisajili hapa kupokea mipasho tunapokaribia Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka wa 2020, ikiwa ni pamoja na live blog itakayokuletea shughuli za siku hiyo.

Coral images courtesy of The Ocean Agency, USFWS, Coral Reef Image Bank, XL Catlin Seaview Survey